MIFUMO PESA NA MAENDELEO YAKE

UTANGULIZI
Pesa ni mfumo utumikao kuwasilisha uhalali wa thamani ya kitu fulani au bidhaa ndani ya miliki , himaya au sehemu fulani.

HISTORIA YA PESA NA MIFUMO YAKE
Hadi sasa pesa imeweza kupitia mifumo mikuu mitano katika matumizi yake ya kufanya biashara ama kununulia bidhaa na mifumo hiyo ni kama ifuatavyo:-
        1      Mfumo wa kubadilishana bidhaa kwa kitu(barter trade)
2 Mfumo wa zana za chuma(iron trade)
3 Mfumo wa karatasi(paper money)
4 Mfumo wa plastiki( credit card)
5 Mfumo wa kidigitali(cryptocurrency) 
 1: MFUMO WA KUBADILISHANA BIDHAA KWA kITU

Biashara ya mabadilishano
Huu ni mfumo uliokuwa mahususi  hapo zamani katika kipindi cha zama za mawe za kwanza ambapo binadamu walitumia njia ya mabadilishano ya kitu kwa chakula kama nafaka , wanyama ilikuweza basi kukidhi mahitaji yao. Hivyo njia ya mabadilishano ilitumika kama mfumo wa pesa.



   2: MFUMO WA ZANA ZA CHUMA
Zama za chuma
Huu ni mfumo ambao binadamu walikuwa wakiutumia kupata vitu kwa mabadilishano ya chuma na bidhaa fulani. Katika kipindi cha zana za kati za mawe mfumo huu uliweza kutumiwa kwa kiasi kikubwa. Kwa lugha ya kitaalamu ulijulikana kama  iron trade system. Wageni kutoka mataifa ya ulaya walikuwa wakija afrika na kufanya biashara hiyo kwa mabadilishano yaliyoelezewa hapo juu. 

3:  MFUMO WA KARATASI
Pesa za noti

Huu umekuwa ni mfumo mama wa pesa hadi sasa ambao unatumiwa dumia nzima na kuwekwa thamani ya uhalali kwenye karatasi ama maarufu kwa jina la noti. Mfano kwa nchi za afrika mashariki ikiwemo Tanzania ambao wanatumia tsh Kenya wanatumia ksh na Uganda wanatumia pia ugsh.


   4: MFUMO WA PLASTIKI


Kadi ya benki
Vile vile pesa haikuweza kuishia hapo ikaja hadi kwenye mfumo wa  plastiki yaani hapa inakuwa katika mfumo wa kadi ujulikanao kama credit card. Hapa mabenki ndio wahisika wakuu wa mfumo huu. Pia unasaidia kupunguza idadi ya kiasi kikubwa cha pesa kukaa katika sehemu salama na rahisi kuhifadhika. 

5: MFUMO WA KIDIGITALI 
Pesa ya kidigitali( Bitcoin)


Maendeleo ya teknologia na maendeleo ndio yaliyopelekea kuingia kwa pesa mpya zilizokuwa katika mfumo wa kidigitali yaani kwa lugha ya kitaalam tunaita cryptocurrency. 
Mfumo huu wapesa uliweza kufanikiwa kutumika mnamo mwaka 2009 na jamaa aliyejulikana kama Satosh Nakamoto mjapani mwenye asili ya kiamerika wakati aliponunua pizza 2 kwa thamamani ya aina ya pesa aliyoitumia iliyokuwa ikijulikana kama Bitcoin ambazo kwa idadi ya thamani zake ilikuwa  Bitcoin elfu kumi.  Hadi sasa hakutaka kujulikana kama ni yeye mwanzilishi wa hiyo aina ya pesa kwa sababu alinukuu na kusema hiyo ni pesa ambayo inamilikiwa na watu wote wa ulimwengu huu. 
Hadi sasa Bitcoin ndio pesa iliyokuwa na thamani kubwa  duniani ukilinganisha na mifumo mingine ya pesa.

Comments

  1. This is official blog for sharing ideas

    ReplyDelete
  2. Replies
    1. Thanks for your co operation๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ

      Delete

Post a Comment